BurudaniUncategorized

Exclusive: Mtanzania ‘Emanuel Austin’ ashindwa kuvumilia, amtaja mmiliki wa chuo cha Ujerumani (+Audio)

Mtanzania ambaye ni mwalimu wa dansi (Choreographer) nchini Ujerumani, Emanuel Austin amefunguka kuhusu mmiliki halali wa chuo cha Tanzschule Weiss cha dansi kilichopo mjini Frankfurt ambacho kimekuwa kikiibua maswali mengi.

Akiongea na Bongo5, Austin amesema kuwa chuo hiko kipo kwa takribani miaka 60 iliyopita na wao wamekuwa walimu hapo kwa miaka kama 10 lakini walifanikiwa kukinunua chuo hiko.

Austin ambaye pia ni msanii wa muziki, amesema kwa sasa yeye na mke wake Larissa Bertsch ndio wamiliki halali wa chuo hiko.

Katika kuthibitisha hilo, msanii huyo ametuma kipande cha gazeti kubwa nchini Ujerumani liitwalo Offenbach Post, akionyesha moja ya stori ambazo zimewahi kuandikwa kuhusu chuo hiko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents