Burudani

French Montana aahidi kuachia albamu yake mpya mwezi Julai

Baada ya muda mrefu kupita bila ya kuwa na albamu sokoni, hatimaye rapper French Montana ametangaza ujio wa albamu yake mpya.

Albamu hiyo ambayo imepewa jina la Jungle Rules, inatarajiwa kutoka Julai 14 ya mwaka huu. Rapper huyo alisema hayo wakati akitumbuiza katika jukwaa la BET wikiendi iliyopita.

Mara ya mwisho Montana aliachia albamu yake ya Excuse My French, Mei 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents