Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Mourinho afunguka kuhusu picha ya Nemanja Matic

Kuna uwezekano mkubwa Nemanja Matic akatangazwa kama mchezaji mpya wa Manchester United muda wowote. Kocha Jose Mourinho ameamuwa kuweka wazi baada ya picha ya kiungo huyo wa Chelsea kusambaa mitandaoni ikimuonyesha akiwa amevalia jezi ya Manchester United.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Valerenga uliofanyika Osl ambao United imeibuka na ushindi wa mabao 3-0, Mourinho amesema mchezaji huyo anatamani sana kujiunga na mashetani hao wekundu wa Old Traford.

“I am waiting for news. I know that he (Matic) wants that very, very much,” amesema Mourinho kwenye mkutano huo. “When a player wants it very, very much, the chance is bigger. I think we have a chance but in football until it’s official – I saw so many things happen that I refuse to say more than I am telling you now.”

Uhamisho wa mchezaji huyo kujiunga na United unatajwa kuwa unaweza kufikia dau la paundi milioni 45. Matic na Diego Costa ni miongoni mwa wachezaji walioachwa na kikosi cha Chelsea kilichopo barani Asia kwa ajili ya mechi za kujipima nguvu.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW