Burudani

Nimefungua record label nikiwa ndani ya RockStar4000 – Barakah The Prince

Baada ya kuachana na record label ya RockStar4000, na kuaanzia label yake ‘Bana Music’, msanii wa Bongo Flava Barakah The Prince amesema label hiyo ilianza kipindi kirefu.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa label hiyo kwa sasa inamsimmaia Naj ambaye kwa sasa ameshatoa wimbo ‘Utanielewa’, pamoja na yeye na kuna wasanii wengine wapya watasikika.

“Bana Music ni label yangu, idea ya kuanzisha record label yangu nipo nayo miaka mingi sana, sema utendaji kazi wake umeanza baada ya kuwa RockStar, yaani nimefungua record label nikiwa ndani ya RockStar,” amesema.

“Msanii wa kwanza Bana music kusimamia wimbo wake alikuwa ni lord Eyes lakini msanii wa kwanza official under Bana ni Naj, pia mimi kazi zangu zitakuwa zinafanywa chini Bana na kuna wasanii wapya nimeshawasaini,” ameongeza Barakah.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents