Vurugu za Hispania kuikosesha Barcelona La Liga?

Kwa muda mrefu wananchi wa Jimbo la Catalonia nchini Hispania wamekuwa wakidai uhuru wao na kuhitaji kujitawala wenyewe kwa kupiga kura za kujitenga na nchi hiyo.

Kabla ya hapo jana wakazi wa eneo hilo kufanya uchaguzi wa kuhitaji kujitenga na Hispania, mwezi Novemba mwaka 2014 Catalonia ilifanya uchaguzi wake usiyoramsi na watu zaidi ya milioni mbili walipiga kura.

Catalonia ni moja wapo ya eneo leyenye ustawi mkubwa wa kiuchumi na eneo la kihistoria nchini Hispania wakati historia yake ikianzia miaka1,000 iliyopita kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ilikuwa sehemu yenye uhuru kabla ya kuingia katika udikteta wa Gen Francisco Franco miaka ya 1939-75 Franco alipofariki taifa hilo lilifufuliwa upya.

Jimbo hili la Catalonia linaundwa na Mikoa minee ambayo ni Barcelona, Girona, Lleida, na Tarrangona wakati Barcelona ndiyo mkoa mkubwa zaidi na sehemu ya kibiashara huku eneo hilo likiwa na Kilometa za mraba 32,108 huku ikiwa na jumla ya watu 7,522,596 kwa takwimu za mwaka 2016.

Karibu soka

Na hapa ndipo ninapokuja kuangazia ni kwa namna gani soka la nchini Hispania litakavyobadilika kwa namna moja au nyingine endapo Catalonia itapata uhuru wake.

Katika miaka ya hivi karibuni, mashabiki wa Barcelona wamekuwa wakionyesha hisia zao hadharani na kuonyesha kile wanachokiamini wakiwa na bendera ya Catalonia na kuingia katika michezo mbalimbali wakati timu hiyo ikiwa inacheza.

Catalonia ni jimbo ambalo hupatikana klabu tatu zinazoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’ ambazo ni FC Barcelona, Espanyol na Girona hivyo kujitoa kwake Hispania kutaziathiri timu hizo.

Njia mbadala wa La Liga ingekuwa ni kutazama ni kwa kiasi gani wanaweza kurejesha Ligi ya Catalan ‘Catalan league’ ambayo ingeweza kujumuisha timu za Barcelona, Espanyol, Girona na nyinginezo ambazo tayari zipo chini ya muamvuli wa mpira wa Hispania lakini ikiongozwa na Shirikisho la mpira wa miguu la Catalonia ‘Catalan Football Federation.’

Waziri wa michezo wa Catalonia, Gerard Figueras amesema “Klabu ya FC Barcelona inaweza kujiunga na Ligi yoyote itakayohitaji kama ni Ligi Kuu nchini Uingereza ‘Premier League’ Ligi ya Ufaransa ‘Ligue 1’ ama Ligi ya Itali ‘Serie A,’ amesema Figueras.

Figueras ameongeza “Ligi nyingi barani Ulaya zinatimu ambazo si zakutoka katika nchi hizo mfano ni Swansea City iliyopo ligi ya Uingereza wakati inatoka Wales na nyingine nyingi kama vile Wrexham kutoka Wales na Newport County ambayo inatoka Wales ya Kusini ndivyo hivyo hata kwa Ujerumani na Itali ambazo baadhi ya timu zao zinacheza Uswisi.”

Waziri huyo amesema kuwa hafikirii kwamba UEFA inachochote cha kupinga inapoona klabu moja inahamia katika ligi nyingine.

Hata hivyo hii itakuwa changamoto nyingine kwa UEFA, na baadhi ya nchi kwa kuwa itaathiri mashindano ya Klabu bingwa barani Ulaya ambayo yanahitaji timu shiriki kutoka katika Ligi za nchi zao.

Waziri Mkuu wa zamani wa Ufaransa, Manuel Valls mwaka 2015 alipendekeza klabu ya Barcelona kushiriki katika ligi ya nchi hiyo Ligi 1 mpaka pale Catalonia itakapo pata uhuru wake kutoka kwa Hispania.

Valls, ambaye ni mzaliwa wa Barcelona alikiambia chombo cha habari cha Journal du Dimanche kuwa kama Monaco inacheza Ligue 1 kwanini ishindikane kwa Barcelona ?.

Don Balon  kwa mujibu wa ripoti ya Don Balon baada ya Catalonia  kupata uhuru wake kuna uwezekano mkubwa  mchezaji raia wa Argentina, Lionel Messi  kuikacha timu hiyo kutokana na kukosekana kwa ushindani wa ligi na hivyo kuhofia kushindwa kuwa bora pamoja na maswala ya kisiasa.

Wanachama wa klabu ya FC Barcelona wameunga mkono vuguvugu la wanachi kutaka kujitoa Hispania.

Watu mashuhuri na maarufu nao wamekuwa wakitoa kauli zao juu ya uhuru wanaoutaka kutoka Hispania miongoni mwa hao ni Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola ambaye anaunga mkono Catalonia kupata uhuru wake mwezi Juni kocha huyo wazamani wa Barcelona alisema kuwa Jumuiya ya kimtaifa ihunge mkono juhudi hizo.

“Tumejaribu mara kadhaa kufikia makubaliano na jibu siku zote limekuwa hapana,” amesema Guardiola.

“Hatuna chaguo tena zaidi ya kupiga kura tunahiyomba Jumuiya ya kimataifa ituunge mkono pamoja na wanademokrasia ulimwenguni watuunge mkono katika kutafuta uhuru wetu,” amesema.

Wakati wachezaji wa Barca, Gerard Pique akiwa ni miongoni mwa watu wanaojisikia fahari kubwa kwa Catalonia kupata utambulisho wake kupitia mtandao wake wa Twitter.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Hispania tayari baadhi ya wachezaji wameshaonyesha wanapohitaji kucheza kama vile Guardiola, Xavi, Carles Puyol na Cesc Fabregas.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW