Yanga SC waache kulalamika imefika kipindi wawe na viwanja vyao – Waziri Mwakyembe

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa kombe la shirikisho Afrika ambao Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 4 – 0 dhidi ya Gendarmerie Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa amefurahishwa na matokeo yaliyopatikana huku akiwataka Yanga SC kuacha kulalamika na badala yake waweke akili yao zaidi katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya St Louis.

“Ni bahatika kuiyona mechi ya leo, ilikuwa nzuri sana unaiyona Simba SC kama timu ambayo kweli ilikuwa kambini na ina mwalimu na uwelewano wa hali ya juu.”

“Mechi ulikuwa nzuri sana nimefurahia na kama kiwango cha mchezo wa mpira Tanzania kitakuwa hiki kama alivyosema mzee wetu Ali Hassan Mwinyi sisi siyo tena kichwa cha mwendawazimu ila cha muungwana ambacho kila mtu lazima akisogelee kwa uwangalifu mkubwa sana.”

Waziri Mwakyembe alipo ulizwa kuhusu malalamiko ya Yanga SC kukosa nafasi ya kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi yao ya kimataifa dhidi ya St Louis amesema

“Niwashauri Yanga SC kwamba akili yao yote ikazanie mechi ya marudiano inayo kuja waache mambo ya kulalamika hakuna dawa hakuna muarubaini ya kushinda ni mazoezi na timu kuweza kuelewana nimeona gonga safi za leo za Simba SC kwa kweli nimeona goli zaidi ya saba ila kwa bahati mbaya sana yamekwenda manne.”

“Kuhusu Yanga SC kulalamika sisi hatujapata malalamiko rasmi ila nimeyaskia bungeni watu wakisema lakini cha msingi ni kwamba wote mnajua uwanja wetu wa taifa umetoka kwenye ukarabati mkubwa sana tumekabidhiwa ukiwa na garantii wa kuweza kuutumia kwa zaidi ya miaka 10 bila kuweka nyasi mpya lakini una masharti yake.”

“Huwezi ukawa na mechi kubwa tatu kwa wiki katika uwanja huu ukifanya hivyo hatuwezi kuwa nao kwa zaidi ya miaka mitatu ijayo.”

“Kilichotokea wiki hii tulikuwa na mchezo wa Azam FC na Simba SC wiki hii moja, huku tukijua tuna mechi mbili za kimataifa na katika mchezo huo timu ngeni inapewa kipau mbele katika uwanja ule ule ambao niwa wenyeji kwa upande wa timu hizi Yanga SC na Simba tulichukulia wana ujua.”

Waziri Mwakyembe amezitaka klabu hizi kongwe Yanga SC na Simba SC ambazo zina umri wa zaidi ya miaka 80 kuwa na viwanja vyao.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW