Izzo Bizness aeleza anavyojisikia kutokana na kuendelea kusahaulika kutajwa kwenye tuzo!
Rapper Izzo Bizness amesema hana kinyongo na waandaji wa tuzo kutokana na kuendelea kusahaulika kutajwa kila mwaka licha ya kufanya kazi nzuri.
Izzo amesema anaamini kusahaulika kwake kunatokana na makosa ya kibinadamu ya watu wanaochuja orodha ya wanaowania tuzo hizo.
“Unaweza ukaangalia labda umepiga video kali, video imepata mapokezi mazuri, lakini sometimes inabidi kuelewa tu kwamba hata hao wanaokaa kuchagua ni binadamu pia,” Izzo ameiambia Bongo5.
“Suala la mimi kutokuchaguliwa ama kuwekwa hata kucompete maybe katika watu kumi bora kwamba tupate watu watatu pia nakuwa sipo, lakini kazi zangu ni nzuri na zimepokelewa vizuri mtaani, naona ni mistake tu za hawa watu wanaoenda kufanya machaguo ya mwisho,” ameongeza.
Izzo amesema hawezi kukata tamaa na anaamini ipo siku kazi zake zitatuzwa pia.
“Kitu ambacho kinaendelea kuja kwangu ni kuendelea kufanya kazi nzuri na kutoa kwaajili ya watu.”