Burudani

Video ya Kcee ft. Diamond ‘Love Boat’ kutoka Ijumaa hii

Diamond anaendelea kujiwekea uhakika wa kuonekana mara nyingi zaidi kwenye vituo mbalimbali vya runinga Afrika kwa kipindi hiki, kupitia video yake pamoja na zile alizoshirikishwa ambazo zinazidi kuachiwa.

kcee na diamond

Kwa sasa video zinazomhusu Diamond ambazo zinaendelea kupata rotation ya kutosha kwenye vituo mbali mbali vya Afrika na nje ni ‘Nana’ pamoja na ‘Nakupenda’ aliyoshirikishwa na Iyanya, ambazo zote zilitoka mwezi mmoja uliopita.

Video nyingine itakayoongezeka kwenye rotation ni ya staa wa Nigeria Kcee na Diamond ‘Love Boat’ ambayo itatoka Ijumaa hii.

“Love boat video will be out on Friday ft @diamondplatnumz, you will love it” ameandika Kcee Instagram.

Kama hiyo haitoshi, video mpya ya collabo ya Donald wa Afrika Kusini na Diamond iliyofanyika wiki iliyopita inaweza kutoka siku si nyingi kama alivyosema Donald katika moja ya Interviews alizofanya wiki iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents