Michezo

Azam FC yaachana na Yahaya Mohammed

Habari kutoka ndani ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC zinasema kuwa imefikia makubaliano ya kuachana na mshambuliaji raia wa Ghana, Yahaya Mohammed.

Uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuufahamisha umma kuwa umefikia makubaliano ya kuachana na mshambuliaji raia wa Ghana, Yahaya Mohammed.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili kufanyika siku ya Jumatatu na Jumanne, ambapo muda wowote kuanzia sasa Mohammed anatarajiwa kurejea nchini kwao Ghana kuanza maisha mapya ya soka nje ya Azam FC.

Azam FC inamtakia kila la kheri mshambuliaji huyo katika masiha mapya ya soka huko aendako na itamkumbuka kwa mambo kadhaa aliyoifanyia Azam FC ikiwemo kushiriki kwenye mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mwaka huu visiwani Zanzibar.

Imekuwa ni kawaida kwa maisha ya soka wachezaji kutoka sehemu moja na kuhamia sehemu nyingine, na itakumbukwa kuwa wakati tunamsajili Mohammed Desemba mwaka jana wakati akiichezea Aduana Stars, alikuwa ni miongoni mwa washambuliaji bora nchini Ghana baada ya kuwa mfungaji bora namba mbili kwa mabao yake 15 nyuma ya Latif Blessing aliyekuwa kinara kwa mabao 17, lakini kinyume na matarajio yetu ameshindwa kuonyesha kile tulichokitarajia awali.

Tunawaomba mashabiki wa Azam FC waendelee kuwa watulivu kwa kipindi hiki wakati tukiwa katika mapambano ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), tunawaahidi kwa kushirikiana na benchi letu la ufundi tutalitumia vema dirisha dogo la usajili linalotarajia kufunguliwa Novemba 15 mwaka huu kuziba nafasi hiyo ya ushambuliaji.

Ni imani yetu mtaendelea kutuunga mkono katika kipindi hiki ambacho tunahitaji kushikamana kwa ajili ya kumalizia vema mbio za kuwania ubingwa wa ligi, tunaamini kwa umoja wetu tutafikia malengo tuliyojiwekea na kuendeleza kauli mbiu yetu ya Timu Bora, Bidhaa Bora.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents