Burudani

BBA Hotshots: Rwanda na Namibia zatolewa, Mganda aokolewa na nchi 4 ikiwemo Tanzania

Rwanda imetolewa kabisa kwenye shindano la Big Brother Africa ‘Hotshots’ baada ya mshiriki wake aliyekuwa amesalia Frankie kutolewa Jumapili November 9.

Frankie

Namibia nayo imeliaga shindano hilo baada ya mshiriki wao wa mwisho aliyekuwa amebaki Permithias kutolewa. Frankie na Permithias walipata kura moja moja tu.

permithias

Ellah wa Uganda ameponea chupuchupu kwa kupigiwa kura na nchi nne Tanzania, Kenya, Uganda na Ghana.

Hadi sasa ni washiriki 12 ambao tayari wametolewa ndani ya siku 35 za mchezo wa kuwania dola 300,000 ambazo zitakabidhiwa kwa mshindi mmoja atakayejulikana siku ya 63.

Hivi ndivyo kura zilivyopigwa:

Butterphly: Malawi, Zimbabwe
Frankie: Rwanda
Ellah: Ghana, Kenya, Tanzania, Uganda
Nhlanhla: Botswana, South Africa
Permithias: Namibia
Trezagah: Mozambique, Nigeria, Rest of Africa, Zambia

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents