Burudani

BBA The Chase: Kwa mara ya kwanza washiriki watatu tu katika dangerzone, Kenya wamo tena!

Zikiwa zimebaki siku 33 tu kitita cha $300,000 cha Big Brother kipate mwenyewe, kwa mara ya kwanza katika The Chase wiki hii kutakuwa na washiriki watatu tu katika kikaango cha Biggie ambao kati yao ni mmoja tu ndio atakayewaaga wenzake siku ya Jumapili ( July 27) katika eviction show.

Annabel
Annabel

Annabel (Kenya), Sulu (Zambia) na Elikem (Ghana) ndio washiriki pekee ambao wamebaki katika dangerzone wiki hii na kufanya eviction ya wiki hii kuwa ya kwanza yenye washiriki wachache (3) na pia itakuwa eviction ya kwanza kutoa mshiriki mmoja atakayerudi nyumbani. Katika Eviction zilizopita idadi ya washiriki watano hadi saba ndio waliokuwa wanaingia kikaangoni na wawili kati yao ndio wamekuwa wakiondoka mchezoni kila jumapili. Jumla ya washiriki 16 wameshatoka na waliobaki ni 12 tu mpaka sasa.

Elikem
Elikem

Leo ni siku ya 58 ya shindano hilo na Tanzania ni moja ya nchi ambazo bado zina washiriki wote wawili mpaka sasa Feza na Nando ambao wako salama tena wiki hii.

Sulu
Sulu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents