Burudani

Big Brother Updates: Angelo, Dillish na Bimp ndiyo wanaopigania uhai wao katika katika ‘The Chase’ wiki hii

Ikiwa ndio wiki ya mwisho ya ‘possible eviction’ katika Big Brother Africa tayari kitendawili cha washiriki wanne waliobahatika kuingia fainali ya The Chase kimeteguliwa.

bba
Jana (August 12) ndio ilikuwa siku ya nomination ambapo Elikem (Ghana), Dillish (Namibia) na Beverly (Nigeria) ndio waliokuwa wamependekezwa kuingia kikaangoni wiki hii, na kilichokuwa kikisubiriwa ni mababdiliko ya mkuu wa nyumba Elikem kutumia nguvu yake ya ‘save and replace’ kuweza kujiokoa na kumuweka mshiriki mwingine kikaangoni.

Kama ilivyotarajiwa na wengi, Elikem aliplay smart kwa kujiokoa yeye mwenyewe na nafasi yake kumuweka Angelo wa Afrika Kusini ambaye anaonekana kuwa tishio endapo atabaki kwenye fainali basi atatoa upinzani mkubwa hasa kwa Elikem. Kumbuka kila mshiriki siku ya jana alipiga kura kwa kuwarushia mishale ya moto wenzake anaohisi watamuongezea ugumu kuufikia ushindi endapo wataingia fainali pamoja.

Baada ya mabadiliko hayo sasa washiriki ambao tayari wamefanikiwa kupata tiketi za kuingia fainali ni Elikem aliyekuwa wa kwanza toka wiki iliyopita mara baada ya Biggie kumtangaza kuwa atakuwa HOH wiki hii. Wengine ni Cleo, Beverly baada ya kuokolewa na Elikem pamoja na Melvin.

Sasa kazi imebaki kwa Afrika kuamua ni yupi kati ya Dillish, Angelo na Bimp atafanikiwa kubaki na kukamilisha Top 5 itakayoingia fainali. Mpaka hapa unaweza kuanza kuhisi ni nani ana nafasi kubwa ya kuondoka na $300,000 za Biggie wiki ijayo?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents