Technology
China yapeleka chombo cha Shenzhou-11 angani, kitaa kwa mwezi mzima
Baada ya miezi kadhaa ya maandalizi, China imepeleka chombo chake chenye wanajimu wawili angani.
Chombo hicho kiitwacho, Shenzhou-11 kilipaa angani kutokea Jiuquan Satellite Launch Centre kwenye jangwa la Gobi.
https://www.youtube.com/watch?v=P7RgtGyaNZo
Wanajimu, Jing Haipeng na Chen Dong watatumia siku mbili kufika kwenye maabara ya Tiangong-2 au ‘Heavenly Palace-2′, iliyoanzishwa September.
Watakuwa huko kwa siku 30 – kipindi kirefu zaidi kwa wanajimu wa China kukaa angani kufanya majaribio ya teknolojia za anga.
Maabara ya Tiangong-2 ipo umbali wa kilomita 393 kutoka duniani.