Burudani

Crazy GK awahimiza wasanii kuitangaza Tanzania kwenye video zao

Rapper King Crazy GK amesema ni busara kwa wasanii wa Bongo Flava kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania katika video zao badala ya kutangaza mazingira na vivutio vya mataifa mengine.

14717567_1809907489288661_1520464086876291072_n

Kupitia kipindi cha The Splash kinachosikika kupitia Ebony FM, GK amesikika akisema kuwa, “Tanzania kuna vitu vingi sana vya kustaajabisha,ambavyo mara chache unaweza kuvipata nje kuna Mlima Kilimanjaro kuna vitu vya akina Mkwawa kuna vitu vingi ambavyo ukivionyesha dunia ina wonder.”

GK ameongeza, “Mzuri pesa umeiona nilimchukua Director wenye exposure nikashoot katika location ambazo wanazitumia wanamuziki wa kawaida hapa Tanzania lakini nilivyozitumia kila Mtanzania ameshangaa. Tuitambulishe zaidi Tanzania kimataifa tayari wenzetu South Africa wameshajitangaza tunaongezea kuwatangaza.”

https://www.youtube.com/watch?v=4mWcHk6kPzQ

Hivi karibuni GK aliachia wimbo wake uitwao Mzuri.

BY CHRIS BEE

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents