Burudani

Designer Makeke apata dili jingine la ‘Rwanda Cultural Fashion Show’

Designer Makeke apata dili jingine la mitindo nchini Rwanda baada ya kufanya vizuri kwenye tamasha la East Africa Fashion Week lililofanyika nchini Kenya mwezi uliopita.

12994426_10205980163811671_7407854058805625659_n

Joctan Makeke maarufu kama Makeke ambaye ni mmoja kati ya madesigner wanaofanya vizuri kwenye mitindo kwa sasa na ameiwakilisha vizuri Tanzania Kimataifa kwenye mitindo, amefanikiwa kupata mualiko mwingine nchini Rwanda kwenye tamasha la ‘Rwanda Cultural Fashion Show’.

Tamasha hilo lililoandaliwa na World Economic Fund na Benki kuu ya Rwanda litafanyika Mei 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa Goethe Institute.

Hongera sana brother Makeke, mafanikio yako ni maendeleo kwa taifa la Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents