Burudani

Dully Sykes: Promota anayetaka kunipandisha ndege lazima tuandikishane kwenye bima ya maisha

Usafiri wa ndege ndio usafiri wa hara zaidi, lakini kwa Dully Sykes ndio usafiri ambao anaouogopa na kuukwepa katika maisha yake kiasi cha kuwa tayari kukataa show ambayo itamlazimu kupanda ndege.

Dully_Sykes

“Sikurogwa wala nini ni tatizo tu linalowatokea watu wengi sio mimi pake yangu”. Dullysykes ameiambia 255 ya XXL ya Clouds FM.

Dully amesema promota yoyote wa nje atakayetaka kumpa show itamlazimu ampe bima ya maisha na kukubali kuihudumia familia yake kwa maisha yote kama sharti moja wapo la kukubali kupanda ndege.

“Mimi naweza kupanda ndege naweza lakini kwasababu nahofia naweza nikafa ndege ikidondoka, basi sio mbaya kwa promota ambaye anataka kunichukua anipandishe ndege tuandikishane tu kwenye bima (life Insurance). Chochote kikitokea ajali aweke saini yake atahudumia familia yangu.”

Dully amesema tatizo lake la kuogopa kupanda ndege ni ugonjwa ambao amedai ameambiwa linatibika kwa kupanda lifti.

“Ishu yangu ya kupanda ndege ni tatizo niliambiwa na wana saikolojia wanasema ni ugonjwa unaitwa phobia,ndio ugonjwa ambao niko nao, unatibika lakini hautibiki kwa vidonge niliambiwa niwe napanda lifti kupanda na kushuka kupanda na kushuka lifti ndefu”.

Dully Sykes ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Serengeti Fiesta Moshi Jumamosi hii, lakini bila shaka hatapanda ndege kwasababu wakati anapewa show za Fiesta alisema hataenda mkoa wowote ambao usafiri ni ndege.

“nakumbuka Dully wakati amekabidhiwa show za Fiesta alisema kwamba mi sitaenda mkoa wowote ambapo usafiri ni ndege, kwahiyo mimi nipangieni mikoa ya karibu karibu ambao usafiri ni gari”, alisema B-Dozen.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents