Burudani

‘Hello’ ya Adele yavunja rekodi nyingine ya Billboard

Mwimbaji wa Uingereza, Adele anaendelea kuweka historia kupitia wimbo wake mpya ‘Hello’.

adele-25-cover

Ikiwa ni wiki moja na siku nne toka ‘Hello’ iachiwe rasmi Oct.23, wimbo huo umeweka rekodi nyingine.

Wimbo huo umevunja rekodi ya Billboard kwa kupakuliwa mara milioni 1.1, na kuwa ndio wimbo uliopata downloads nyingi zaidi ndani ya wiki moja. Rekodi hiyo hapo awali iliwekwa na wimbo wa Flo Rida ‘Right Round’ wa mwaka 2009, uliopata downloads 636,000 ndani ya wiki moja.

Wakati huo huo ‘Hello’ pia imekamata namba 1 kwenye Billboard Hot 100 wiki hii.

‘Hello’ ni single ya kwanza kutoka kwenye album mpya ya tatu ya Adele, ‘25’ inayotarajiwa kutoka Nov.20.

Wimbo wa Justin Bieber ‘Sorry’ ndio unaofata katika nafasi ya 2 kwenye Billboard Hot 100, Digital Songs, na Streaming Songs charts.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents