Technology

Instagram yaboresha huduma yake ya ‘Instagram Direct’

Habari njema kwa watumiaji wa mtandao wa kushare picha wa Instagram ni kuwa, huduma ya ‘Instagram Direct’ sasa imeboreshwa zaidi.

Instagram Changes Terms Of Service, Stirs Anger Among Users

Instagram Direct ni huduma inayowawezesha watumiaji kuweza kutumiana picha, video na ujumbe binafsi kwa mtu mmoja, au kundi la watu atakaowachagua mwenyewe bila mtu mwingine kuona.

insta 2

Hivi sasa kuna ki mshale kimeongezwa pembeni mwa icon ya like na comment chini ya kila post. Kazi yake ni pale utakapoipenda picha au post ya mtu unaweza kumtumia mtu kwa kukibonyeza kimshale hicho kwa kutumia Instagram direct.

insta 3

Pia hivi sasa uwanja wa kuchat wa Instagram direct umepata muonekano unaofanana kama wa Messenger.

Katika maboresho hayo pia sasa hakuna ulazima wa kumtumia picha mtu ili uweze kuanza kuchat nae kwa ujumbe, ukiwa kwenye uwanja wa Instagram direct, unaweza kuchagua ‘send message’, kasha unachagua jina la unayetaka kumtumia kwa kusearch jina lake na kuanza kumuandikia ujumbe moja kwa moja bila picha.

Ili kuyaona mabadiliko hayo mtumiaji anatakiwa ku update app ya Instagram kwenye simu yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents