Technology

Instagram yaja na feature mpya ya ‘stories’ kama ya Snapchat

Instagram imeanzisha kitu kipya kuwafurahisha zaidi watumiaji wake.

15593835-bb2b-433c-8290-b87a8cd86733 (1)

Imeanzisha feature ya ‘stories’ inayoonekana juu kabisa ya app hiyo inayowezesha picha na video kuwekwa muda huo huo na kukaa kwa masaa 24.

Katika jitihada za kuwafanya watumiaji wawe na desturi ya kupost mara kwa mara kuhusu maisha yao, kuanzishwa kwa stories kutakuwa na mabadiliko makubwa kwa matumizi ya app hiyo yenye watumiaji milioni 300 kila siku.

Stories, iliyoanza kuonekana kwa wengi Alhamis hii kwenye mifumo ya Android na iOS, imefanana kwa kiasi kikubwa na Snapchat ambapo unaweza kurekodi video kwa sekunde hadi 15. Tofauti na Snapchat, unaweza kubonyeza post upande wa kushoto wa screen kurudisha picha za nyuma.

Kama ilivyo kwenye Snapchat, unaweza kujibu stories kwa message na zitaonekana kwenye inbox ya Instagram Direct. Kuna kimshale kinachoelekea juu ambacho ukikigusa utaona orodha ya watu ambao wameona ulichoweka. Unaweza pia kublock watu ambao hutaki waone ulichoweka.

Kama akaunti yako ya Instagram ni public, bado story yako ni public pia na unaweza pia kuona story public za mtu bila kumfollow kwa kubonyeza picha zao za profile.

Na kama umeridhishwa na post zako za story, unaweza kuzipost kwa njia ya kawaida kwa kubonyeza vinukta vitatu vilivyopo chini kulia kwenye screen na kushare.

Kutengeneza post za story, bonyeza alama ya jumlisha iliyopo kushoto mwa app. Unaweza kuongeza maneno, kuchora na kuweka mbwembwe zingine kwenye picha au video yako.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents