Bongo5 Makala

Kwanini Congcong Wang aliyeshika nafasi ya pili kwenye matokeo ya kidato cha nne amekuwa habari kubwa?

Kuna mjadala unaendelea kwanini, Congcong Wang, Mtanzania mwenye asili ya kichina aliyeshika nafasi ya pili kwenye matokeo ya kidato cha nne anapewa coverage zaidi kuliko hata yule wa kwanza.

12750117_235803580095223_1028821096_n
Congcong Wang (kushoto) akiwa na mama yake pamoja na mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, Barbara Hassan

Watu wanahisi kuwa Congcong Wang amepewa coverage zaidi kumzidi Butogwa Charles Shija Canossa Girls aliyeshika nafasi ya kwanza.

Uandishi wa habari au journalism ni taaluma kama zilivyo sheria, udaktari nk. Ina principles zake kama fani zingine. Kuna vitu vinaitwa news values ambazo ni kama principles za kufanya habari iwe habari.

Nitazieleza hizi chache ambazo ni kubwa kwa ufupi ili kwa wale wasiofahamu waelewe kwanini habari zingine ambazo kwa mtazamo hudhani hazina uzito.

1. Impact

Habari ambazo zinawagusa watu wengi zaidi hupewa kipaumbele. Mfano Tanesco ikitangaza mgao wa umeme nchi nzima. Hii ni habari ambayo kila mtu inamhusu.

2. Conflict/Controversy

Habari zinazohusu migogoro, ugomvi, vita, mikwaruzano huteka attention za watu.

3. Proximity (Ukaribu)

Watu hupenda kusoma habari zinazowahusu kwa ukaribu wake. Mfano Tanesco ikitangaza mgao wa umeme Kinondoni, habari hii haimhusu mtu aliyepo Bukoba.

4. Timeliness

Habari za wakati huu. Mfano ajali ya pikipiki ya leo iliyosababisha kifo cha mtu mmoja kwa msomaji inaweza kuvuta hisia kuliko ajali ya gari iliyoua watu watatu lakini ilitokea wiki tatu zilizopita.

5. Prominence

Habari za watu maarufu hupewa uzito zaidio. Ndio maana habari za Diamond, Alikiba, Wema Sepetu na mastaa wengine zimetawala

6. Human Interest/Emotion

Habari zinazogusa mioyo ya watu, habari za huzuni nk.

7. Unusualness – Mambo yasiyo ya kawaida

Kuna usemi maarufu sana kwenye uandishi wa habari kuelezea principle hii, kwamba ‘mbwa akimuuma mtu sio habari. Lakini mtu akimuuma mbwa, hiyo ni habari.

12717121_880278615422367_1064327844_n

Sasa habari ya Congcong Wang kushika nafasi ya pili kwenye matokeo ya kidato cha nne inaingia kwenye ‘Unusualness.’ Hili si jambo la kawaida. Ni jambo ambalo halijawahi kutoka Tanzania kwa mwanafunzi ambaye wazazi wake wote wawili ni Wachina, licha ya kuzaliwa Tanzania ameshika nafasi hiyo ya pili kwenye matokeo ya kidato cha nne.

Tena cha kushangaza zaidi ni kuwa amepata B kwenye somo la Kiswahili. Wote tunajua kuwa raia wengi wa kigeni hasa Wachina huongea zaidi lugha zao na wengi hawajui hata Kiswahili cha kuombea maji.

IMG_20160219_110025_625
Congcong Wang akihojiwa kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV

Hakuna shaka kuwa katika familia ya msichana huyu lugha ya mawasiliano inayotumika zaidi ni Kichina. Kuna maswali mengi zaidi ya kuuliza kuhusu amewezaje kuwa mjuzi wa Kiswahili kwa kuzingatia mazingira anayoishi na shule aliyosomea. Feza Girls ni miongoni mwa shule za kishua zaidi Tanzania na hutumia Kiingereza kufundishia.

Hiyo ina maana kuwa hata alipokuwa shule, Kiingereza ndio lugha aliyokuwa akiitumia zaidi kuzungumza na wanafunzi wenzake. Labda kama familia yake inaishi kwenye maeneo ya kawaida ambapo na uwezo wa kujichanganya na waswahili kiasi cha kumpa uwezo wa kukifahamu zaidi.

Ninavyofahamu mimi ni kuwa familia za aina hii huishi kivyao zao na mara nyingi huwa hazina mazoea na familia za wazawa. Kwa sababu hizo ndio maana Congcong Wang anaendelea kupata coverage ya kutosha. Hiki sio kitu cha kawaida!

Ninachukua fursa hii kumpongeza pia Butogwa Charles Shija (kwenye picha hapo chini) kwa kuongoza matokeo hayo.

Number-1

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents