Burudani

Linex ndani ya bongo movie, ashiriki katika filamu mpya ya Aunty Ezekiel ‘Mwajuma’

Msanii Linex Sunday Mjeda aka The V.O.A ameamua kufungua ukurasa wa pili wa kipaji ambacho hajawahi kukionesha cha uigizaji, hivi karibuni ataonekana katika filamu mpya ya muigizaji wa bongo movie Aunty Ezekiel inayoitwa ‘MWAJUMA’.

linex na Aunty Ezekiel

Akiongea na Bongo5 leo, Linex amesema filamu ya Mwajuma imebeba story ya msichana aliyekuwa na maisha ya kawaida na baadaye kuja kuwa na maisha mazuri yaliyopelekea tabia yake kubadilika na kuanza kubadili wanaume.

“Movie inaitwa Mwajuma, Mwajuma alikuwa mama ntilie tu wa mgodini maisha yakamnyookea akawa anabadilisha wanaume kama nguo.” Alisema Linex

linex na Aunt Ezekiel

Katika movie hiyo ambayo ndiyo ya kwanza kwa msanii huyo wa ‘Kimugina’, Linex amecheza kama mmoja wa wanaume waliopangwa foleni na Mwajuma, “So mimi ni ni mmoja wa wanaume wa Mwajuma niliyebadilishwa kama nguo”. Alisema Linex

Mwajuma1

Mwajuma2

mwajuma3
Huyu ndiye Mwajuma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents