Habari

Maiti inayotembea yaleta kasheshe Manzese

polis4_face

 

 Bakari Hamisi  anayekadiliwa kuwa katika ya miaka 20 na 25, aliyefariki juzi saa moja usiku amezua mtafaruku mkubwa baada ya maiti yake kugomewa kwenda kuzikwa kwenye makabuli ya Jumuiya pale Manzese.




Kijana huyo ambaye  alianguka ghafla wakati akicheza mpira katika viwanja vya Faru, vilivyopo karibu na kituo cha polisi Mpakani Manzese, kabla ya kufikwa na mauti akiwa kwao.

Mshuhuda mmoja  wa makamo,  amesema baada ya kuosha maiti hiyo kwa la kuupeleka msiki wa Kione na kuuzikwa kwenye makabuli ya  Msikiti wa Jumuiya Manzese kwa mfuga mbwa, ndipo kundi la watu walipokuja kwaajili ya kuzuia.

pilisi_1

Watu hao walidai kwamba marehemu, ameonekana akitembea mtaani, jambo ambalo lilipelekea watu wengi kujaa eneo hilo. Kauli hiyo ilizidi kuenea kwa watu waliokuwa msibani, na hatmaye  kujaa na kila upande wa msikiti kwa lengo  kupinga  kuzikwa kwa mwili huo, ambao wanadai si mwili harisi kwakuwa mtu huyo yupo hai na wamemficha kimazingara

polisi3

Taarifa hiyo inasema ndipo polisi wakaamua kuingilia kati, suala hilo ambalo tayari lilionekana kuwa ngumu. Hata hivyo, baba wa marehemu mzee Hamisi alitangaza msikitini mwili ukazikwe, lakini vijana walikwenda kufukia kaburi na kuzuia mwili huo usifike hapo.

Polisi ilibidi watumie kupiga hewani sisasi  ilikuwatawanya, jambo ambalo lilipelekea watu hao kuanza kurusha chupa , mawe na magongo  ya miti.Polisi wamefanikiwa kuuchukuwa mwili wa marehemu na kuupeleka kwenye hospitali ya Mwanayamala.

 polisi8

polisi_2

 

polisi_5

polisi_6

polisi_7

Wananchi wakiendelea kuzuia mwili wa marehemu usiende kuzikwa, kwa madai mpaka wamtoe akiwa hai.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents