Habari

Makamu wa Rais akutana na ujumbe wa SHIMUTA (+Picha)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMUTA) mjini Dodoma.

Akizungumza baada ya kikao na Makamu wa Rais, Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Khamis Mkanachi alisema wamekutana na Makamu wa Rais na kumkabidhi ripoti ya mashindano ya mwaka 2016-2017 na 2017-2018.

Pamoja na kumkabidhi Ripoti hiyo, pia walimueleza Makamu wa Rais ambaye ni Mlezi wa Shirikisho, changamoto na mipango mbali mbali ya kuboresha shirikisho hilo.

Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents