Uncategorized

Mesut Ozil kushuka dimbani kuikabili BATE Borisov, baada kukosa michezo 20, Unai Emery amtaka apambane na hali yake

Huwenda kule kutoelewana baina ya kocha wa Arsenal, Unai Emery dhidi ya nyota wake Mesut Ozil kukafikia tamati hii leo baada ya nyota huyo kuwepo na matumaini makubwa ya kucheza kwenye mechi yao na BATE Borisov.

Meneja huyo wa Arsenal amemtaka Ozil kuamka na kuhakikisha anafanya mazoezi ili aweze kuwa futi yatakayomfanya kujihakikishia nafasi ya kucheza ndani ya kikosi chake.

Arsenal manager Unai Emery appears to be running out of patience with flaky Mesut Ozil, telling him to train with consistency and start producing some performances

Ozil ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi ndani ya klabu hiyo ambayo ni pauni 350,000 kwa wiki huku akiwa si chaguo la Emery baada ya kutowekwa kwenye michezo kadhaa iliyopita.

Akizungumza kuelekea kwenye mchezo wao wa UEFA Europa League dhidi ya BATE Borisov utakaopigwa hapo baadae, Emery ameweka wazi kuwa amefanya mazungumzo na mchezaji huyo raia wa Ujerumani.

”Kwenye mazungumzo yetu nimemtaka kuwa na muendelezo mzuri, kuwa tayari kwaajili yetu kwenye mazoezi ili kuwa fiti,” amesema Emery.

Emery ameongeza ”Endapo utafanya mazoezi kwa kujituma na muendelezo mzuri utatusaidia kwenye mechi, nimekuwa nikimuangalia kwenye mazoezi na bado tunamuhitaji na nafahamu hata yeye anahitaji hilo.”

” Lakini anahitaji kuwa na muendelezo, kuwa mtu amabaye anaweza kupatikana kila anapohitajika kwenye mechi pasipo kuwa na majeraha wala kuumwa hapo ndipo tunaweza kumuona Mesut aliyebora.”

Ozil amekuwa akiingizwa akitokea benchi kwenye michezo 18 ya mashindano yote msimu huu huku kutoshiriki jumla mechi 20. 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents