Picha

Mwanafunzi bora kidato cha sita 2015/16 akabidhiwa tuzo yake ya ASSA2016

Mwanafunzi aliyeongoza katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2015/16 nchini, Ramadhan N.Gembe wiki hii alikabidhiwa rasmi cheti chake cha tuzo za wanafunzi bora AfriKa Mashariki, ASSA 2016.

63ffa381-4d73-4e26-875b-f124f8cabd6a
Ramadhan N.Gembe (kushoto) akikabidhiwa na Dj Aaron cheti chake baada ya kushinda tuzo za ASSA 2015/16

Gembe amekabidhiwa cheti chake wiki hii kutokana na kukosekana wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo zilizofanyika July 29 mwaka huu kufuatia kubanwa na masomo.

78522bde-41f9-4276-9efe-9b5b928c7a27

Aaron ambaye ni mmoja wa waasisi wa tuzo hizo amesema kwa sasa wanandaa msimu wa pili wa ASSA, ikiwa ni pamoja na kuanzisha kipindi cha TV chenye lengo la kuleta hamasa ya masomo kwa njia ya elimu na burudani (edutainment) kwa vijana wa Afrika ambao bado wako mashuleni.

7ecf5ba5-e54c-4fed-82b6-4f913d5788e1
Dj Aaron akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba baada ya mazungumzo

“Kipindi hiki ni sehemu ya kazi za kuelekea tuzo za wanafunzi bora, ambazo kilele chake ni mwezi Juni mwakani 2017,” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents