Burudani

Penzi la Moni Centrozone na mpenzi wake ‘Nai’ ngoma nzito

Penzi la msanii Mone Centrozone na mpenzi wake, Nai lipo katika hali mbaya.

Taarifa zilizopo ni kwamba wawili hao wamekuwa katika ugomvi wa mara kwa kile kinachoelezwa kuwa Moni ana mwanamke mwingine nje ya mahusino yao na pindi anapoulizwa na anatoa kipigo kwa bibie, Nai.

Nai ambaye ni video vixen maarufu Bongo ameiambia E-Newz ya EATV kuwa ugomvi wake na Moni umeshafika hadi kwa mama yake mzazi, hata hivyo mwenzake haoneshi nia ya kutaka kumaliza jambo hilo.

“Nishamuomba msamaha nishampigia simu, Moni nipo kwa mama hapa ongea naye. Moni kachukua ile simu ya mama yangu kaikata na mama yangu kampigia hajapokea,” amesema.

Utakumbuka Nai alitokea katika video Moni na Roma inayokwenda kwa jina la Usimsahau Mchizi. Nai alipata umarufu mkubwa pale alipotokea kwenye video ya Darassa iitwayo Muziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents