Habari

Prof Tibaijuka aeleza kwanini hakuzichukua mil 200 za tuzo Marekani

Hivi karibuni, Waziri wa zamani wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka alidaiwa kuzikataa zaidi ya shilingi milioni 200 alizotakiwa kupewa baada ya kushinda tuzo ya kimataifa ya ‘His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award for Sustainable Development’ nchini Marekani.

tibaijuka-1

Na sasa Profesa Tibaijuka, amekanusha uvumi huo na kutoa ufafanuzi kwanini hakuzipokea.

“Kilichotokea kwenye hii tuzo wanayosema nimekataa, haina tofauti na pesa za Rugemalira tena hii ni mbaya zaidi, hela za Rugemalira hazikuwa za kwangu, zilikuwa ni kupeleka shuleni au siyo, na nilizipeleka wakati wa kampeni, nilikuja nama audit report au sio, niliwaonyesheni.Sasa tuzo hii ina vipengele vitatu, kuna cheti nimekileta, kuna likopi lizito liko Dar es Salaam siku ya kidedea ntalileta Mungu akipenda. Ilikuwa pia na tuzo ya fedha,dola laki 1 takribani milioni 200 na ushee,” alifafanua.

“Sasa nikawaambia wale wanaotoa tuzo asanteni sana, sikukataa fedha,hawa watu wa Dar es Salaam wengine hawanitakii mema, eti nimekataa fedha sikuweza kuzichukua,kwasababu za kisheria,lasivyo haya haya ya Escrow ndio yangenikuta,”, alisema Tibaijuka.

“Sasa hawa nikawaambia sikiliza kule kwetu sheria ni ngumu, kwahiyo hizi fedha mimi naziacha hapa hapa mezani, tukajipanga na nikawaambia kule kwetu kuna maafa, kule kwetu kuna shule, kule kwetu kuna maabara,kule kwetu kuna vijana, ninyi kama mnaweza kuwasaidia hizi fedha itabidi ziende moja kwa moja kwao,tuko pamoja? Nikizipokea mimi ndio hayo hayo mambo ya Escrow. Mimi mwenyewe nimeziacha zile hela kwa masikitiko makubwa au siyo. Tunahangaika hapa na Saccos, tunahangaika na maabara, tunahangaika na madawati, mimi nilikuwa mtu wakuacha hela pale mezani,” alihoji.

“Lakini sheria imenifunga na watu wengine wanasema ‘ameziacha kwanini’ kwasababu ningezichukua ingekuwa ni kizungumkuti. Sheria ya maadili inasema kiongozi haruhusiwi kuchukua zaidi ya shilingi elfu 50, ukichukua elfu 50 mimi nipo chini ya mheshimiwa spika wa bunge, natakiwa nibebe zile hela nipeleke kwa spika. Kwahiyo nazikabidhi. Sasa sheria ya maadili inasema elfu 50 na zaidi unapeleka serikalini hiyo inaonekana safi. Unaweza ukapeleka, sheria ya kodi inasema unapopata fedha yoyote ni mapato yako, kwanza unalipa kodi. Ndio nikasema jamani wanaosema hela huwezi kuzikataa, ntazikataaje wakati tuko katika shida ya matetemeko, madawati na shida chungu nzima?”

BY:EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents