Technology

Top 20 ya majiji yanayotweet zaidi Afrika, Dar es salaam ni ya 12

Portland Communications imetoa orodha ya miji na majiji 20 yanayo-tweet zaidi barani Afrika katika utafiti waliouita ‘How Africa Tweets study’.

twitter2

Jiji la Johannesburg ndilo linaloongoza kwa geo-located tweets 344,215 ,l ikifuatiwa na mji mwingine wa Afrika Kusini, Ekurhuleni kwa tweets 264,172.

Cairo imeshika nafasi ya tatu 227,509 ikifuatiwa na Durban ya Afrika Kusini.
Kwa upande wa Afrika Mashariki jiji la Nairobi ndilo linaloongoza, huku likikamata nafasi ya sita katika top 20, huku Dar es salaam ikiwa kwenye nafasi ya 12 kwa tweets 22,581.

Portland ilifanya uchambuzi wa geo-located tweets za kutokea Afrika katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho wa mwaka jana (2013).

Pia matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa siku za Jumanne na Ijumaa ndio ambazo watu wengi hu-tweet kote ulimwenguni.

Hii ni orodha kamili (Top 20)

Johannesburg – 344,215
Ekurhuleni – 264,172
Cairo – 227,509
Durban – 163,019
Alexandria – 159,534
Nairobi – 123,078
Cape Town – 83,818
Accra – 78,575
Abidjan – 56,054
Douala – 51,441
Lagos – 44,392
Dar es Salaam – 22,581
Kano – 19,023
Ibadan – 13,703
Algiers – 12,317
Kinshasa – 10,201
Luanda – 7,312
Addis Ababa – 3,307
Dakar – 788

Source: Portland Communications

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents