Habari

Utafiti wa Twaweza wabaini wanafunzi lukuki wanaomaliza shule bila kujua kusoma

Utafiti uliofanywa na taasisi ya Twaweza mwaka 2014 na kupewa jina la ‘Uwezo’ unaonesha kuwa mamilioni ya wanafunzi nchini, humaliza elimu ya msingi bila kuwa na uelewa wa masomo ya darasa la pili lakini pia kukiwa na changamoto kadhaa ikiwemo ni utoro wa walimu na upungufu wa vifaa vya kujifunzia.

image

Ripoti ya utafiti huo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam, inaonesha kuwa kati ya watoto 32,000 waliopimwa katika kaya 16,000, asilimia 54 wanafunzi wa darasa la tatu hawajui kusoma hadithi nyepesi ya darasa la pili, wakati asilimia 16 ya wanafunzi wa darasa la saba hawajui kusoma hadithi za darasa la pili.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, alisema, “Watoto wengi sana Tanzania hii hawana uwezo stahiki wanapomaliza darasa la pili hata pale watakapomaliza darasa la saba, na kumaliza elimu ya msingi bado unaweza kuona mmoja kati ya watoto wanne au watano hawana sifa au vigezo vya kuingia kidato cha kwanza, kusoma kufanya hesabu, Kiingereza na Kiswahili. Hili nadhani ni tatizo tulilonalo kila mwaka.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents