Habari

Video: Rais Magufuli aiunganisha familia ya Masaburi msibani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli, ameiunganisha familia ya aliyekuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam, marehemu Dk Didas Masaburi, wakati akizungumza msibani.

c6

Kwenye tukio hilo lililogeuka gumzo mtandaoni, Rais Magufuli aliwatambua wajane wengine wa marehemu ambao hawakutajwa kwenye wosia.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwapa pole wafiwa wote, ninafahamu alitajwa mke wa marehemu mmoja,mimi nafahamu wake wa marehemu wako wanne watano hivi,” alisema Rais wakati wa kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

https://www.youtube.com/watch?v=Ibv3kUgmrqQ

“Katika tabia zetu za kiafrika kuwa na wake zaidi ya wawili, watatu, wanne, watano kumi ni kitu cha kawaida,”alisisitiza. “Kwahiyo napenda nichukue nafasi hii kuwapa pole sana wake wote wa marehemu Masaburi, pamoja na watoto wote wa marehemu. Inawezekana tukazungumza watoto wako 20 lakini mimi najua watoto wako zaidi ya 20,” aliongeza na kusababisha shangwe kutoka kwa waliokuwa wakimsikiliza.

Pia aliwaasa kuwa na umoja katika kipindi hiki ambacho wamempoteza kichwa cha familia.

c1

“Na mimi nitoe wito kwa wanafamilia hasa watoto mara nyingi panapotokea msiba shetani huwa anacheza mchezo wake. Ninawaomba nyinyi watoto mkashikamane, mkamtangulize Mungu. Baba yenu aliwapenda, mkifarakana mtaleta mateso makubwa kwa marehemu Masaburi kwasababu aliwapenda wote, hakuwabagua na ndio maana hata mahali pa kwenda kuzika amechagua mahali pa wote.”

“Narudia niwaombe sana sana watoto mkishikamana nyinyi mama zenu watashikamana na ndugu wanaohusiana wote watashikamana, kwahiyo kwa mtoto mkubwa aliyetangulia kuzaliwa na marehemu Masaburi ukawe kiongozi wa familia.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents