Habari

Video: Serikali yaweka mkakati kukabiliana na upungufu wa Maziwa nchini

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.Dk Charles Tizeba amesema serikali imeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini.

Hayo yamesemwa na Dk Tizeba, wakati akijibu swali la Mbunge wa Wete Mhe.Mbarouk Salum Ali, Bungeni MJini Dodoma lililohoji Je, Tanzania ina mbuzi wa ngapi pamoja na ng’ombe wa maziwa wangapi?

“Nakubaliana na Mhe.Mbunge kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya mifugo lakini bado kuna upungufu wa maziwa,ambapo takwimu za makadirio za mwaka 2016 zinaonyesha lita bilioni 2.09 za maziwa zilizalishwa na unywaji wa maziwa kwa mtu kwa mwaka ulifikia lita 47 ukilinganisha na lita 200 zinazopendekezwa na Shirika la chakula Duniani”,alisema Mhe.Tizeba

Aidha kati ya Ngombe milioni 28.4, Ngombe rasmi wa maziwa ni 782,995 tu sawa na asilimia 3 ya Ng’ombe wote.Aidha kati ya mbuzi milioni 16.7 ni mbuzi rasmi takribani 50,000 ndio wa maziwa ambao ni asilimia 0.3 ya mbuzi wote.

Hata hivyo alitaja jitihada ambazo Serikali imechukua ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini ni pamoja na kumarisha mashamba ya kuzalisha mifugo ya Serikali (LMU’s) ili kuongeza idadi ya Ng’ombe wenye uwezo wa kuzalisha maziwa kwa wingi.

Aidha alisema Serikali imeanzisha vituo vya uhimilishaji katika kanda 6 hapa nchini ambazo ni kanda ya Ziwa(Mwanza),kanda ya Magharibi(katavi),Kanda ya kati(Dodoma),Kanda ya Mashariki(Kibaha),Kanda ya Kusini(Lindi) na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini(Mbeya) kwa lengo la kutoa huduma ya uhilimishaji wa Ng’ombe wa Maziwa walioko kwenye maeneo hayo pamoja na Ng’ombe wa Asili ili kuzalisha idadi kubwa ya Ng’ombe wa Maziwa.

Video:

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents