Burudani

Video ya wimbo mpya wa Joh Makini ft. AKA ‘Don’t Bother’kutambulishwa MTV Base (Nov.10)

Baada ya Nikki Wa Pili wa Weusi kutambulisha wimbo wake mpya ‘Baba Swalehe’ Ijumaa iliyopita, sasa ni zamu ya kaka yake Joh Makini kuwaonesha mashabiki wake wa Tanzania na Afrika kwa ujumla kile alichoenda kufanya Afrika Kusini miezi kadhaa iliyopita.

Joh na AKA MTV

Video ya wimbo mpya wa Joh Makini aliomshirikisha rapper wa Afrika Kusini ‘AKA’ itatambulishwa kwa mara ya kwanza leo (Nov. 10) saa 12 jioni (saa za Afrika Mashariki) na kituo cha kimataifa cha MTV Base.

‘Don’t Bother’ imetayarishwa na producer Nahreel wa The Industry, na video imeongozwa na director Justin Campos wa Afrika Kusini.

Weusi waliahidi baada ya uchaguzi wataachia kazi zao mpya kwa kupishana siku moja ama mbili. Baada ya Joh na Nikki kutambulisha kazi zao karata itahamia kwa G-Nako ambaye naye ana video ya wimbo wake mpya ‘Original’ ambayo pia alifanyia Afrika Kusini na Campos.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents