Habari

Wajumbe baraza kuu CUF na wabunge hawako tayari kukaa meza moja na Lipumba

Wakati mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akitafuta suluhu ya mgogoro wa siasa unaokikabili chama hicho, wajumbe wa baraza kuu na baadhi ya wabunge, wamesema hawako tayari kukaa naye meza moja wakidai kiongozi huyo alikataa maridhiano wakati wakimuomba asijiudhuru.

lipumba

Akiwa katika ziara mikoa ya Kusini inayojumuisha mkoa wa Lindi na Mtwara, Profesa Lipumba amewaomba wafuasi wa chama hicho kupitia dini zao kukiombea chama chao ili kumaliza tofauti zao na kuanza kukiimarisha chama.

“Tuyamalize basi,mambo yashaharibika,tuzungumze namna ya kurejesha umoja, badala ya kurejesha umoja tunaanza kufukuza uanachama,” alisema Lipumba.

Wakati Lipumba akiomba maridhiano na wajumbe wa baraza kuu na wabunge wa chama hicho, wao wamesema kwa kuzingatia katiba ya chama, hawapo tayari kukaa meza moja na badala yake wanafuata katiba.

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali, alisema “Suala la kukaa kunasiana halikuanza leo, lilianza tarehe 1 mwezi wa 8 2015 kwahiyo watu waelewe hili. Viongozi wa dini, viongozi wa chama viongozi wengine wa madhehebu mbalimbali, walimfuata Profesa nyumbani kwake mimi mwenyewe nikiwa mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wa CUF taifa. Nilikwenda nyumbani kwake, kwa Profesa kwenda kumpigia magoti ‘Profesa usifanye hivyo.’ Lakini siku nne baadaye, tarehe 5 mwezi wa 8 Profesa aliandika barua. Maana yake ni nini, kwamba hii meza anayoihitaji huku kunasiana anakokuhitaji. Mimi nadhani yeye angekubali kwanza tarehe 5 mwezi wa 8 au tarehe 1 tulivyokuwa tunamnasihi usijiuzulu na nyie wote ni mashahidi.”

Kwa upande wake Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka, alisema, “Yeye alipotangazwa na msajili kwamba amemtambua kama mwenyekiti halali angekuwa mtu wa maridhiano alitakiwa sasa amfuate katibu wake aonyeshe uhalali ule, aliingiaje ofisini. Lakini yeye alipopata taarifa kwamba msajili kamtambua, Aliamua kwenda kuvamia ofisi kuvunja milango kuingia na kutangaza kwamba mimi mwenyekiti halali. Sasa mtu anayetaka maridhiano hawezi akaanza na uhalifu halafu arudi kwenye maridhiano.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents