Habari

Waziri Mwakyembe aeleze A-Z safari ya Mzee Majuto kuelekea India (+video)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema safari ya kumpeleka Msanii maarufu nchini King Majuto kuelekea India kupatiwa matibabu umeshakamilika.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa Mzee huyo ataongozana na Mkewe na mwanafamilia mmoja pamoja na Daktari wetu kutoka Wizara ya Afya.

“Nafurahi kusema kwamba mipango ya kumpeleka nje ya nchi Msanii maarufu nchini King Majuto kwa matibabu imeshakamilika, King Majuto akiongozana na Mkewe na mwanafamilia mmoja pamoja na Daktari wetu kutoka Wizara ya Afya, wataondoka hapa siku ya Ijumaa tarehe 4 kwa ndege ya Oman Air ambapo msanii wetu atapata matibabu stahiki,” amesema Dkt. Mwakyembe.

“Tulikuwa na kurupushani sana katika hizi mbili 3, 4 kuweza kukamilisha hati zote za usafiri wale wote wanaosafiri nae, vilevile kupata taarifa za kitabibu sahihi na vile vile wale wenzetu wa India wamejiandaa vipi namna ya kumtibu yote yamekamilika saivi ni kusafiri tu.”

Aidha aliwashukuru wadau wa sanaa hasa tasnia ya filamu kwa kwa kujitoa kwenda Muhimbili kumuangalia mwenzao, pamoja na hayo amewashukuru kampuni mbalimbali waliochangia matibabu ya Mzee huyo.

Sambamba na hilo aliongeza kuwa safari ya majuto kwenda India serikali imebeba mzigo huo asilimia 100 na hata alipokuwa Muhimbili serikali imekuwa ikimuangalia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents