Bongo Movie

William Mtitu atoa neno kwa waliokosa ‘Mama Kubwa’

Muongozaji wa tamthilia ya Mama Kubwa na Jirani, Willum Mtitu ameweka bayana kutokuwa na mipango ya kutengeneza DVD ya tamthilia ya ‘Mama Kubwa’ ambayo imeshaisha.

Akiongea na Bongo5, Mtitu ameeleza kuwa kupitia kampuni ya 5Effect hawana mpango wa kuiweka tamthilia hiyo katika DVD ili kuuza kwa wasio itazama na wanaotaka kuirudia kuitazama.

“Ile tamthilia wakati tunaitengeneza day one hatukufiliria kuitengenezea DVD, kama ulikosa Mama Kubwa basi wewe angalia Jirani kwa sasa, labda hapo mbeleni irudiwe kwa kuonyeshwa ila sio kwa sasa,”amesema Mtitu.

Vile vile Mtitu hakusita kuonyesha furaha yake kwa mapokeao ya tamthilia hiyo ya Mama Kubwa na kueleza kuwa Watanzania wanataka vitu vyenye muendelezo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents