Burudani

Belle 9 aanza kulifikiria soko la kimataifa, atautumia mwaka 2014 kuubadilisha muziki wake ili kufikia malengo hayo

Mwanzo wa mwaka kila msanii huweka mipango mipya ya kazi kwa mwaka husika, upande wa msanii wa R&B Belle 9 kutoka mji kasoro bahari Moro Town, amesema azimio lake (resolution) la mwaka huu 2014 ni mabadiliko makubwa katika muziki wake kama alivyofanya kupitia single yake mpya ‘Wanitaka’ aliyoitoa mwishoni mwaka jana 2013.

belle-9

“Kwa mwaka huu lengo langu kubwa ni kuubadilisha muziki wangu, kwasababu muziki ambao nilikuwa naufanya mwanzo na muziki ambao nimemaliza nao mwaka na ndio ambao nimeanza nao mwaka unatofauti kubwa, kwahiyo kikubwa kutoka kwangu kwa mwaka huu ni changes”.

Akizungumza na Bongo5, Belle amesema pia kwa sasa ameanza kulifikiria zaidi soko la kimataifa,

“Ukiachana na kuhitaji kubadilika mpango wangu mwingine mkubwa ni kutoka nje ya mipaka ndo kitu ninachokifikiria sana, mfano mtu kama Diamond kufanya Collabo na Davido ni mfano mzuri sana kwetu au mtu kama AY amekuwa na jitihada kubwa za kufungua mipaka, kwahiyo focus yangu nyingine kubwa mwaka huu ni kuanza kulitafuta soko la kimataifa.”

Belle 9 amemtaja msanii wa Nigeria May D kuwa ndiye anatamani sana kufanya naye kazi na amekuwa akifuatilia kazi zake japo hajabahatika kuwasiliana naye.

Belle ambaye ni baba wa mtoto mmoja amesema kwa sasa yuko katika mipango ya kufanya video ya wimbo wake mpya ‘Wanitaka’ ambao amedai hajaamua atafanya na nani japo ameishawasiliana na madirector kadhaa wa Tanzania na Kenya ambao wote wameonesha nia ya kutaka kufanya naye video ya wimbo huo, na wengine wamempigia baada ya wao wenyewe kuupenda wimbo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents