Michezo

Mesut Ozil aishika pabaya timu ya Arsenal

Huenda timu ya Arsenal ikapata pigo jingine kutoka kwa Mesut Ozil.

36204

Mchezaji huyo raia wa Ujerumani anaweza akauzwa endapo atakataa kusaini mkataba mpya kutokana na huu aliokuwa nao sasa kumalizika mwaka 2018. Hata hivyo kuna uwezekano mchezaji huyo akarejea kwenye timu yake ya zamani ya Hispania, Real Madrid kutokana na kauli yake aliyowahi kuitoa kuwa yupo tayari kurudi kuichezea timu hiyo.

Ozil na Sanchez wameonekana kumuumiza kichwa kocha Arsene Wenger kutokana na mikataba yao kumalizika pamoja huku mpaka sasa wakionekana kutokuwa na mpango wa kusaini mikataba mipya na timu hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents