Burudani

Diamond, Davido na Yemi Alade kutumbuiza jukwaa moja na Ne-Yo kwenye tuzo za 2015 MTV MAMA

Zikiwa zimebaki siku chache kabla tuzo za MTV Africa Music Awards Kwazulu-Natal-2015 (MAMA) kutolewa, orodha ya wasanii watakaolishambulia jukwaa na kutoa burudani inazidi kuongezeka.

mama mtv

Baada ya msanii wa kimataifa Ne-Yo kutoka Marekani kutangazwa kuwepo, majina ya wasanii wa Afrika watakaotumbuiza yametangazwa.

Kama ilivyokuwa mwaka jana, Diamond Platnumz na Davido wametajwa kutumbuiza kwa mara nyingine kwenye tuzo za mwaka huu.

Wasanii wengine watakaotoa burudani siku hiyo ni Yemi Alade (Nigeria), Cassper Nyovest (South Africa) na Bucie (South Africa).

Tuzo za MAMA zitatolewa July 18, Durban, Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents