Habari

Je wajua kuna wanafunzi wanaoenda chuo/shule kuwaridhisha tu wazazi wao?

Inawezekana sio jambo la kushangaza au wengine wanashangaa kuhusu kichwa cha habari hapo juu. Nimekutana na mmoja wa wanafunzi wa chuo kimoja hapa nchini (jina nalihifadhi) akasema ” Mimi nachukia shule kwa sababu ni kitu ambacho nataka kuwaridhisha wazazi wangu. Wao wanafikiri nikipata shahada ndio nimefanikiwa lakini kwangu si kitu ninachotaka” anasema mwanafunzi huyo.

o-LAZY-HIGH-SCHOOL-STUDENT-facebook

Hebu tujue mambo ambayo anayataja na anayachukia kwenye chuo hicho. anaendelea kusema ” Mwalimu anaingia darasani na laptop yake anaanza kutusomea halafu kipindi kinaisha anaondoka, hapa anasema amefundisha. Hicho ni kitu ambacho angetupa wenyewe tukafanya na hivyo ndivyo tunavyofanya tunajisomea”. mfumo wa vyuo vyetu unakuwa hautusaaidii kujifunza kwani ni kama kunakili kutoka sehemu fulani.

“Haimaanishi vyuo vyote viko katika mfumo huo au walimu wote wako hivyo bali mimi naenda chuo niwaridhishe wazazi wangu na nikimaliza nitaendelea na mambo yangu ambayo nimeyapanga kufanikisha,” aliendelea kusema mwanafunzi huyo.

Jambo la Kujiuliza, Je wazazi wanajua kwanini watoto wao wako shule?

Kama huyo ni mwanafunzi mmoja anafanya hivyo, inamaanisha wazazi wengi hawajui kitu gani watoto wao wanataka. Hivyo wanafikiri wanawasaidia kwenda shule, na mtoto anajaribu kumridhisha mzazi. Ni wakati sasa wazazi kuchukua jukumu la kujua watoto wanataka wafanye nini kwenye maisha na kuwasaidia katika maeneo hayo. Haimaanishi watoto wasipate elimu ya msingi, hapana baada ya elimu ya msingi je mtoto ana ndoto gani juu ya maisha yake?

Jambo la Pili , Je mfumo wa ufundishaji wa Vyuo vyetu unasadia?

Tumekuwa na wimbi la vyuo vingi hapa nchini, na inabidi kujiuliza kama mfumo wetu unasaidia wanafunzi kufikia malengo yao. Na ukitaka kujua kama mfumo unatusaidia inabidi tuchunguze wanafunzi wetu wanaomaliza vyuo wanaweza kufanya nini kwenye soko la ajira. kama hawawezi kufanya kazi ya kile walichosomea hu vyuoni, tunatengeneza kizazi ambacho kitaendelea kusumbua nchi kwa kutokua na ujuzi unaokidhi mahitaji yetu.

Jambo la Tatu, walimu au wakufunzi wetu hamshituki kwamba soko la ajira linabadidika na unahitaji kubadilika?

Ni ukweli unaouma, bali kama unafundisha au unalipwa kwa wewe kuwasomea wanafunzi kitu ambacho ni darasa la kwanza au chekechea ndicho wanachofanya hakuna unachokifanya. Heshima na taaluma yako itadharauliwa na kila mwanafunzi atakayepita kwako.

Mwisho, wanafunzi wanatakiwa kutambua kwanini wapo hapo walipo kabla ya kuchukulia mambo kawaida. Kwa kila mwanafunzi anatakiwa kujitizama ni kitu gani anatakiwa kukifika au ana malengo gani ambayo yatamfikisha kule anakotaka kufika na kuwashirikisha wazazi au walezi na kuona kitu gani kinaweza kufanyika.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents