Burudani

Msechu atoa somo kwa wasanii ambao hawafanikiwi licha ya kutoa kazi kila siku

Peter Msechu ni msanii ambaye hua haoni tatizo kukiri mapungufu yake hadharani, kama ilivyo kwa wasanii wengine wa muziki wa Bongo ambao huwa wanashindwa hata kutaja watu wanaowasaidia mfano kwenye uandishi wa nyimbo zao.

Msechu

Kupitia Instagram, Msechu ameandika ujumbe mrefu akiwashukuru Amini na Barnaba kwa sababu wamehusika kwa sehemu kubwa katika mafanikio aliyonayo kimuziki.

Muimbaji huyo wa ‘Nyota’ pia ametoa ushauri kwa wasanii wote wadogo na wakubwa kukubali mapungufu yao pasipo kuficha, na kuomba msaada kwa watu wengine wenye uwezo katika yale ambayo wao hawawezi kufanya.

Hiki ndicho alichoandika Msechu:

“SIJUI NIANZIE WAPI ILA NAFIKIRI NENO MOJA TU ASANTENI SANA SANA KWA UWEPO WENU HAPA DUNIANI NA HASA KWENYE GAME HII YA BONGO FLAVIOUR!!
Nimeanza mziki huu mara tu baada ya kutoka bss 2009 hapo katikati nimetoa nyimbo nyingi sanah zaidi ya 14 zipo zilizofanya vizuri kiasi chake kama hasira hasara na relax angalau zikasikia ila zipo ambazo pia sikuwahii kuzisikia tena zilikufa mara moja mara tu baada ya kutoka!! Kifupi sikuwahi faidi mziki wangu toka nianze kazi hii!!

NAMSHUKURU MUNGU mwaka jana mwanzoni ikatokea kufanya kazi na AMINI @amini_tz ambaye sijui alitokea wapi yeye akaniletea beat melody na kila kitu ikazaliwa #NYOTA Kwa kweli asante sana bro hapo ndio nilianza ona faida ya kuwa mkweli na kuwaachia wenye kazi zao wafanye!! Nyota ndio nyimbo pekee iliyofanya vizuri sanah sana na pekee ndio nyimbo niliyoona pesa ikiingia! Ilinipa wakati mgumu baada ya nyota nini kitafata sikukata tamaa ya kusema kuwa sina uwezo wa kuandika hit song.

MUNGU si athuman barnaba akaniambia peter naomba nikupe kitu!! Kuanzia melody maandishi kila kitu @barnabaclassic akaamua kupoteza muda wake week nzima akiniandikia #MALAVA sijui nisemeje kwa kweli Namuona mungu kwa kweli juu ya mziki wangu kwa sasa na kwa kweli naweza sema MLILETWA DUNIANI KWA AJILI YANGU BROZ @amini_tz na @barnabaclassic ASANTENI SANA SANA SANA SANA KWA KUNISAIDIA NA KUNITOA PALE NILIPOKUWA NA SASA ANGALAU WAKISEMA WASANII WENYE HIT SONG WATOKE MBELE KWA KWELI NITAKUWA MSTARI WA MBELE! Asanteni sana tena sana na nawaombeni msinichoke nitakuja tena na tena!!!

KWA WASANII WADOGO AMA WAKUBWA AMBAO BADO WANAJIULIZA KWANINI HAWAFANYI VIZURI NA WANATOA KAZI ZAO KILA SIKU NAFIKIRI JARIBU KUJIULIZA KIPI UNAWEZA NA KIPI HAUWEZI WAACHIE WATU WANAOWEZA WAKUSAIDIE!! Usihangaike kutafuta mchawi!! UNAWEZA KUWA MWANDISHI MZURI ILA HUNA MELODY UNAWEZA UKAWA UNAJUA MELODY ILA SIO MCHAGUZI MZURI WA BEATS KUBALI KUPATA MAWAZO MAPYA UTAFIKA MBALI!!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents