Uncategorized

Picha: Kisa Gor Mahia, Mbao FC yatikisa jiji la Mwanza, mapokezi yake hajawahi tokea tangu kutinga ligi kuu

Uongozi wa klabu ya Mbao umewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kujitokeza kwao kwa wingi mno kuwapokea baada ya kutua Mwanza wakitoka Dar es salaam kwenye michuano ya Sportpesa.

Wingi huo wa mashabiki umechagizwa na timu yao ya Mbao FC kuifunga miamba ya soka ya Kenya Gor Mahia licha ya kutofanya vizuri kwenye mashindano hayo kutokana na kushika nafasi ya nne ikitolewa na Kariobangi Sharks hatua ya nusu fainali.

Kupitia akaunti yao ya kijamii wa Instagram uongozi wa Mbao FC umetoa shukrani zao za dhati kufuatia mapokezi hayo makubwa hayajawahi kutokea kwa timu hiyo.

”Uongozi wa Mbao Fc unatoa shukurani nyingi za dhati kwa Wapenzi na Mashabiki wa Mbao Fc kwa kuipokea kwa kishindo timu yao pendwa,” Uongozi huo umeandika ujumbe huo.

Hata hivyo uongozi wa Mbao FC umeongeza ”Hii ni ishara tosha tuliweza kuwakilisha vyema mkoa wetu wa Mwanza katika mashindano ya @tzsportpesa Cup 2019.”

”Tunaahidi kuendeleza moto huu Ligi kuu Tanzania bara ikiwa mungu akiendelea kutupa uzima na nguvu kwa Viongozi, Wachezaji na Benchi la ufundi.Kikubwa ni kuendelea kuipa support timu haswa hamasa yenu Uwanjani tuwapo na mechi.”

Mbao FC ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya kuwatoa mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya Sportpesa timu ya Gor Mahia kisha na wao kuondolewa na Kariobangi Sharks kabla kupata kipigo kutoka kwa Simba SC kuwania nafasi ya tatu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents