Picha

Under The Same Sun wamtuza Fid Q

fid q (600x578)

Taasisi ya Under The Same Sun inayojihusisha na kutetea haki ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino nchini, imemtunuku rapper Fareed Kubanda ‘cheti cha shukrani’ kwa mchango wake katika kampeni ya shirika hilo.

Fid amepost picha akiwa na mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa shirika hilo la nchini Canada, Peter Ash na kuandika, ‘Just received CERTIFICATE OF APPRECIATION from the one and only Mr Peter Ash( CEO of Under The Same Sun ).’

“Mwaka jana nilijumuka na UTSS ktk ziara yao ya kanda ya ziwa nikiwa kama muelimishaji kwenye vita dhidi ya mauaji ya ALBINO,” Fid ameiambia Bongo5 kupitia Twitter.

“Kujituma kwenye uchapaji kazi na utaratibu wa kuwa na nidhamu kazini ni moja kati ya vitu vilivyomfurahisha sana Mr Peter Ash,” ameongeza Fid.

Hongera sana Fid.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents