Burudani

Video ya Mrs Superstar ya Young Killer Msodoki kutoka rasmi leo (February 21)

Hatimaye video iliyokuwa ikiuliziwa na kusubiriwa kwa hamu ‘Mrs Superstar’ ya rapper kutoka jiji la miamba Mwanza, Young Killer Msodoki inatarajiwa kutoka rasmi leo Ijumaa (February 21).

young killer mrs superstar

Video hiyo ambayo ilishootiwa mwezi November mwaka jana (2013) itaachiwa katika vituo vyote vya TV pamoja na mtandaoni muda wowote leo.

Akizungumza na Bongo5 producer na meneja wa Young Killer Mona G amesema walikuwa pia na mpango wa kufanya uzinduzi rasmi wa video hiyo, lakini zoezi hilo halitaweza kufanyika kutokana na kukosa ukumbi.

“Ilikuwa tufanye launch kabisa lakini kila ukumbi tuliojaribu kuulizia tunaambiwa una event, yaani kumbi zote zimeshakuwa booked so imekuwa ngumu” amesema Mona. “Video tumekabidhiwa toka juzi tunayo lakini leo ndio tunaitoa kote kwenye TV na blogs”.

Video ya Mrs Superstar ambayo imefanyika katika mazingira ya studio pamoja na maeneo mengine ya nje, imeongozwa na Adam Juma wa Visual Lab/Next Level.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents