Uncategorized

Zari afunguka haya na kueleza jinsi alivyoutumia mwaka 2018 kurekebisha baadhi ya makosa yake

Mwanamama Mjasiriamali, Zari ambaye pia ni mzazi mwenzie na msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abduly alimaarufu Diamond Platnumz amefunguka mwanzo mwisho jinsi alivyopitia katika miaka miwili yaani 2017 na 2018 na kusema yuko tayari kwa ajili ya 2019.

Zari kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka na kueleza matatizo yote yaliyomkuba mwaka 2017 ikiwemo kuondokewa na Mama yake mzazi pamoja na aliyekuwa mume wake Ivan.

Lakini pia ameeleza jinsi alivyoutumia mwaka 2018 katika kujemga na kuyarekebisha baadhi ya makosa yake na matatizo aliyopitia pia kujijenga zaidi baada ya kuondokea na wapendwa wake hao wawili na kuahidi kuwa yuko tayari kwa mwaka 2019.

“Mwaka 2019 niko tayari kwa mwanzo mpya ….
Katika maisha, sisi huumiza, tunafanya makosa, tunasamehe, tunaendelea. Lakini, zaidi ya yote na kwa njia yote tunayojifunza. Asante 2018, bado nina pumua. #Waliyotegemea #Blessed #Thankful Shiriki nami hadithi yako ya maisha”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents