Lifestyle

Betrice Miss TZ No 3 anavyowakimbia mastaa, eti anadai ni single girl ? (Video)

Mlimbwende @iambeatricealex (22) ambaye ni Miss Tanzania namba 3 mwaka 2022, Miss Ilala mwaka 2022 na Miss Dar namba 2 mwaka 2022, amefunguka kuhusu mipango yake kupitia tasnia yake ya urembo huku akionekana kuwapiga chenga mastaa wa muziki kupitia u-video vixen.

Mrembo huyo amedai amekuwa akipokea ofa za wasani mbalimbali kwaaajili ya kushiriki katika video zao za muziki lakini amekuwa akiwachomelea kwa kuwa sio malengo yake kwa sasa.

Ameyasema hayo Jumamosi hii akiwa Onomo Hotel Posta Jijini Dar Es Salaam muda mfupi baada ya uzinduzi wa mashindano ya Miss Dar Zone ambayo usaili wake utafanyika weekend ijayo.

Amedai wao kama warembo wapya wa kizazi hiki wanataka kufanya vitu tofauti ili kuwavutia mabinti wengine kuona urembo fursa ambayo unaweza kuitumia kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents