Habari

Rais Magufuli atoa agizo kwa Halmashauri zote nchini

Halmashauri nchini zimetakiwa kuhakikisha zinaanzisha mifuko ya dawa na vifaa tiba ili kurahisisha upatikanaji wa huduma katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati katika maeneo yao.

Agizo hilo limetolewa leo, Maei 2 na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.

Rais Magufuli amesema kuwa kuanzishwa kwa mifuko hiyo kutasaidia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa urahisi kwakuwa halmashauri zitakuwa na uwezo wa kununua moja kwa moja kupitia fedha zitakazotokana na mifuko hiyo.

“Natumia fursa hii kuziagiza Halmashauri zote nchini kuanzisha mifuko ya dawa na vifaa tiba (Drug Funds), hili isaidie katika kurahisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika maeneo yenu”, alisisitiza Rais Dkt. Magufuli.

Aliongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba Serikali imetenga Sh.50 Bilioni katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2018/19.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents