Habari

Fahamu kijiji ambacho wanaume huzungumza lugha ya tofauti na wanawake

Hakika dunia inamambo mengi na mengine ukisimuliwa huwenda ukashindwa kuamini, kijiji kimoja kilichopo Kusini mwa nchi ya Nigeria kinacho fahamika kwa jina la Ubang wakazi wake wakiume hutumia lugha tofauni na wanawake. Masked men in Ubang performing in a masquerade Wakazi hao jamii ya wakulima wanaume na wanawake hutumia lugha mbili tofauti huku wakielewana na kuamini kuwa hiyo ni baraka waliyobarikiwa na Mungu lakini Kiingereza kikionekana kuanza kupata umaarufu taratibu kwa vijana. Chief Oliver Ibang. Chifu wa kijiji cha Ubang, Oliver Ibang

Kwa mujibu wa ripota wa Shirika la habari la BBC, Yemisi Adegoke ameripoti kuwa Chifu Oliver Ibang akiwa amevalia vazi lake nadhifu za jadi na kofia safi ya rangi ya nyekundu alithibitisha hilo kwa kuwaita mabinti zake wawili na kuwapatia gimbi kisha kuwauliza linaitwaje na kujibiwa bila kusuasua kuwa ni ”irui,” lakini kwa upande wa wanaume gimbi huitwa “itong”. Chifu, Ibang  alitoa mifano mingi mno kama vile mavazi ambayo kwa wanaume wa kiji hicho huita “nki” lakini kwa wanawake kwao huyaita “ariga” . Picha hiyo huonyesha baadhi ya vitu vichache ambavyo wanaume huito kwa lugha ya tofauti na wanawake ikiwa mfano wake ni maji wanaume huyaita ”abu” lakini wanawake wa kijiji hicho huita ”okwakwe”. Community members say the sexes understand each other but only use the language of their sex Mpaka sasa haijafahamika kuwa ni kwa nini wakazi wa kijiji hicho hutumia lugha mbili tofauti kwa kutofautisha jinsia zao. Mtaalamu wa maswala ya kale, Chi Chi Undie amesema kuwa yapo baadhi ya maneno ambayo huwa wanatumia jinsia zote mbili lakini yapo mengine ni tofauti kabisa si kwa kwakuandika na hata matamshi. Pindi watoto wakiume wanapokuwa hutpendelea zaidi kutumia lukha ya wanawake lakini wanapofikia hatua ya balehe hubadilika na kuzungumza lugha ya wanaume na hiyo inakuwa ishara ya kuwa sasa amekuwa na wala hakuna mtu ambaye anaambiwa abadilike.

Related Articles

2 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents